Powered By Blogger

Friday, August 19, 2016

PIGO KWA MZIKI WA TAARABU BI SHAKILA SAID AAGA DUNIA

GWIJI WA MUZIKI WA TAARAB, BI SHAKILA SAID AAGA DUNIA.

MWIMBAJI mkongwe wa taarab aliyeitikisa Afrika Mashariki kwa sauti yake tamu, Bi Shakila Said amefariki dunia usiku huu. 
Kwa mujibu wa  mtoto wa marehemju aitwaye Shani amesema kwamba Bi Shakila amefariki baada ya kudondoka ghafla. 
“Mama hakuwa mgonjwa hata kidogo, aliswali swala ya magharibi vizuri na baadae kidogo akadondoka na kufariki,” alisema Shani huku akilia. 
Bi Shakila amefia nyumbani kwake Charambe jijini Dar es Salaam na mwili wake tayari umepelekwa kuhifadhiwa katika hospitali ya Temeke. 
Kwa mujibu wa Shani, kwa sasa hivi bado hakuna utaratibu wowote wa mazishi uliopangwa. 
Katika uhai wake Shakila alitamba zaidi katika vikundi vya Luck Star na Black Star za Tanga pamoja na JKT Taarab ya Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment