Powered By Blogger

Sunday, October 2, 2016

AMIRI JESHI MKUU RAIS DKT. MAGUFULI ALIPOFUNGA MAFUNZO YA MEDANI YA KIJESHI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akilakiwa na Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Jenerali Davies Mwamunyange alipowasili kushuhudia kufungwa kwa  mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka majini  (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akilakiwa na Mnadhimu mkuu wa JWTZ  Luteni Jenerali Venance Mabeyo  alipowasili kushuhudia kufungwa kwa  mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka majini  (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akilakiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi  alipowasili kushuhudia kufungwa kwa  mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka majini  (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akipeana mikono na Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jenerali Robert Mboma alipowasili kushuhudia kufungwa kwa  mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka majini  (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akipeana mikono naMkurugenzi wa Operesheni hiyo  Meja Jenerali James Mwakibolwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalumu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Haji Omar Kheir akilakiwa na makamanda. Nyuma yake ni Katibu Mkuu Kiongozi wa SMZ  Dkt. Abulhamid Yahya Mzee
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi akiongea na Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jenerali Robert Mboma
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Jenerali Davies Mwamunyange  alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi  alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu  wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt Modestus Kipilimba alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibious Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu   alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibious Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Afande  John Casmir Minja alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibious Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna  Valentino Mlowola alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibious Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na  Kaimu Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Mama  Victoria Lembeli alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibious Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokea saluti toka kwa  Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi   alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibious Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi  alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jenerali Robert Mboma alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Mama suzana Mlawi
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Majenerali wa JWTZ 
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa zoezi hizo Meja Jenerali James Mwakibolwa
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akijiandaa kuweka saini katika kitabu cha wageni akishuhudiwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini katika kitabu cha wageni
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein

Monday, September 19, 2016

FAHAMU HAYA KUHUSU ‘CHAMBUA KAMA KARANGA’ YA SAIDA KAROLI IKIWEMO



 KUTUMIKA KWENYE FILAMU YA HOLLYWOOD

Diamond ameachia wimbo mpya ‘Salome’ aliomshirikisha Ray vanny, wimbo huu umechukua vionjo kwa asilimia kubwa kutoka kwenye wimbo wa ‘Chambua kama karanga/ Maria Salome’ wa Saidi Karoli.Tumeona tukukumbushe mambo ambayo labda hufahamu kuhusu wimbo wa ‘Chambua kama karanga’ wa Saida Karoli. Mbali ya kuwa wimbo huo ulitoka kipindi cha mwaka 2000 mwaka 2013 ulitumika kwenye filamu ya Marekani ya muongozaji maarufu Tyler Perry ‘Peeples
Filamu hiyo imeigizwa na mastaa kama Kerry Washington, Craig Robinson na Malcolm Barrett.Hatahivyo Saida Karoli alidai kuwa hakupokea malipo yoyote kutoka kwa waandaji wa filamu hiyo japo alisema arifurahi kuona kazi yake imepewa heshima ya kutumika kwenye filamu hiyo.
Wimbo huo pia ulibeba jina la Albam ya kwanza ya saida karoli iliyozinduliwa tarehe 2 Septemba mwaka 2001,  ‘Maria Salome’ ni moja ya album za muziki za Tanzania zilifanya vizuri zaidi sokoni.
Mwaka 2012 Saida Karoli alikua msanii pekee wa kike kutoka Tanzania aliyechaguliwa kuwania tuzo za KORA, alikuwa anawania kipengele cha ‘Mwanamuziki bora wa kike wa Afrika Mashariki’

ALICHOKISEMA DIAMOND KUHUSU KURUDIA WIMBO WA SAIDA KAROLI





ALICHOKISEMA DIAMOND KUHUSU KURUDIA WIMBO WA SAIDA KAROLI


Wengi tunajua kwamba wimbo wa “Salome” wa Diamond ni wimbo ambao umetoka katika ngoma ya“Maria salome” sasa je Saida karoli amepata shavu la mtonyo?
Diamond Platnumz Weekend hii ameachia ngoma inaitwa Salome amemshirikisha Rayvanny, na ndani ya wimbo huo wa “Salome” diamond amerudia melody ya ngoma ya “Maria salome” kutoka kwa legendarySaida Karoli, ngoma ambayo ilikuwepo kwenye album ya mwaka 2001 karibu miaka 16 iliyopita.
Sasa Diamond amerudia vitu flani flani hivi ambavyo sio mbaya kumuenzi Bi Dada kwasababu sheria za kimataifa za Hati miliki zinasema kwamba kurudia ngoma ya msanii fulani bila kuulizwa ni mpaka ngoma iwe imefikisha miaka 50 sasa kwa Diamond ilikuwaje?
Diamond amefunguka na kusema kwamba siku tatu nyuma Diamond alishafanya mazungumzo na uongozi wa Saida Karoli kwasababu Diamond yeye kama yeye anasema kwamba anaheshimu kazi ya mtu na hapendi mtu kazi yake aichukulie kwa dharau na vilevile kuna kiasi cha hela ambacho Diamond alikitoa na kutoa share kwake kwamba kila amount ya pesa inayoingia kwenye video hiyo basi Saida naye atakuwa na share yake.Kingine pia ambacho ulikuwa ukifahamu kuhusiana na wimbo huu wa Salome ni kwamba siku ambayo timu ya WCB ilipoalikwa kupata chakula cha mchana kwa Mh Jakaya Mrisho KikweteDiamond alimwoneshaMh Jakaya Mrisho Kikwete hiyo video ya Salome na akatokea kuikubali sana.

NDEGE ALIZONUNUA RAIS MAGUFULI MOJA ITATUA KESHO



Ndege moja kati ya mbili za ATCL Alizonunua Rais Magufuli Itatua Kesho Nchini

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Patrick Itule alisema ndege hiyo aina ya Bombardier Q400 inatarajiwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 7:00 mchana.

Itule alisema ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 76, tayari imeanza safari ya kuja nchini tangu mwishoni mwa wiki iliyopita ikipitia miji ya Reykjavík, Southampton, Malta, Luxor, Addis Ababa Ethiopia kabla ya kutua nchini ikiwa na timu ya marubani wanne kutoka Canada.

“Ndege ya pili inatarajiwa kukabidhiwa Septemba 22 na kuanza safari ya kuja Tanzania Septemba 23,’’ alibainisha

RAIS DKT .MAGUFULI AMJULIA HALI SAMUEL SITTA

 

Rais Dkt. Magufuli Amjulia Hali Spika Mstaafu Samuel Sitta Pia Atembelea Kwa Kushtukiza Ofisi Za Magazeti Ya Uhuru Na Mzalendo Jijini Dar Es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 19 Septemba, 2016 amefanya ziara ya kushitukiza katika Ofisi za Gazeti la Uhuru zilizopo Mtaa wa Lumumba Jijini Dar es Salaam na kuzungumza na wafanyakazi.

Katika Mazungumzo hayo, wafanyakazi wa Gazeti la Uhuru linalomilikiwa na CCM wamelalamikia kutolipwa mishahara yao kwa miezi saba, kutotolewa kwa michango ya wafanyakazi kwa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kuuzwa kwa mtambo wa kuchapisha magazeti katika hali ya kutatanisha, kutotambuliwa katika ajira kwa baadhi ya wafanyakazi, kutolipwa kwa madeni wanayozidai taasisi za Serikali na wanaostaafu kutolipwa mafao yao.

Wafanyakazi hao pia wamemueleza Dkt. Magufuli kuwa Bodi na Menejimenti ya kampuni ya vyombo vya habari vya chama inayoendesha Gazeti la Uhuru na Redio Uhuru zimeshindwa kuendesha vyombo hivyo na wamemuomba aingilie kati ili kuvinusuru vyombo hivyo ambavyo kwa sasa vina hali mbaya kutokana na kukabiliwa na madeni makubwa, na biashara yake imeshuka kwa kiasi kikubwa.

Akijibu malalamiko hayo Rais Magufuli aliyetembelea ofisi za Gazeti la Uhuru akitokea Ofisini kwake katika jengo la Makao Makuu ya chama, Ofisi Ndogo ya Lumumba Jijini Dar es Salaam amemuagiza Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahaman Kinana kuhakikisha mishahara yote wanayodai wafanyakazi inayofikia Shilingi Milioni 609 inalipwa ndani ya Mwezi huu wa Tisa, ameagiza kupatiwa orodha ya taasisi za Serikali zinazodaiwa na Magazeti ya Uhuru na Mzalendo, na pia ameagiza deni linalodaiwa na NSSF kutokana na kutowasilishwa kwa makato ya wafanyakazi lilipwe.

Kuhusu malalamiko dhidi ya Bodi na Menejimenti ya Kampuni hiyo, ajira za wafanyakazi, mafao kwa wastaafu, kuuzwa kwa mtambo wa kuchapisha magazeti na mazingira magumu ya kazi Dkt. Magufuli ameahidi kuyafanyia kazi.

Aidha, Dkt. Magufuli amewapongeza wafanyakazi wa Gazeti la Uhuru kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya licha ya kukabiliwa na changamoto kubwa na amewakikishia kuwa anatambua umuhimu wao na kwamba atahakikishia anaboresha hali ya chombo hicho muhimu.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemjulia hali Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samwel Sitta ambaye anaendelea kupata matibabu Jijini Dar es Salaam na hali yake inaendelea vizuri.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

19 Septemba, 2016 



TFF NA DIAMOND TRUST MAMBO YAMEIVA

Benki ya Diamond Trust (DTB) leo imesaini kuingia mkataba na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kudhamini Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (VPL) kwa msimu wa mwaka 2016/2017.

DTB inaungana na mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) pamoja na wadhamini wengine katika kudhamini ligi hiyo maarufu kama Ligi Kuu ya Vodacom.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla ya utiaji saini huo iliyofanyika Hoteli ya Serena, Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki hiyo, Joseph Mabusi amesema:  “Udhamini huu utasaidia zaidi maendeleo ya soka nchini kwa kuziwezesha timu timu shiriki pamoja na jitihada zingine za TFF. Soka inaunganisha Watanzania wa matabaka mbalimbali ambao ni wateja wetu na si kama benki tungependa kuwa karibu nao zaidi kupitia mchezo huu.”

Mabusi aliongeza kwa kusema:  “Tunafurahi na kujivunia kuwa sehemu ya ligi kuu na tunaamini udhamini huu utazidisha ari ya kuwahudumia Watanzania wote.

Benki ya Diamond Trust imekuwa ikiipa kipaumbele michezo mbalimbali ikiwemo soka, ambapo timu rasmi ya soka inayoundwa na Wafanyakazi imefanikiwa kushinda vikombe na mataji mbalimbali ya soka likiwemo taji la ligi ya mabenki nchini inayojulikana kama BRAZUKA KIBENKI mwaka 2015 pamoja na ngao ya hisani ya ligi hiyo mwaka 2016.

Benki pia inadhamini timu ya soka ya Agathon iliyopo Mbagala inayoshiriki ligi soka daraja la tatu. Zaidi ya hayo benki pia inajivunia kuwa moja kati ya wadhamini wa michuano ya CECAFA Kagame Cup mwaka 2015.

Ligi hiyo inajumuisha timu 16 kutoka Tanzania bara zinazocheza kwa mfumo wa mechi za nyumbani na ugenini ambazo ni Young Africans, Simba Sports Club, Azam FC, Mtibwa Sugar, Kagera Sugar, Mbeya City, Majimaji, MbaoFC, African Lyon, JKT Ruvu, Ruvu Shooting, Tanzania Prisons, Stand United, mwadui FC, Ndanda FC na Toto Africans.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi waandamizi wa Shirikisho la Soka Tanznaia –TFF wakiongozwa na Rais wao Ndugu Jamal Malinzi, Wafanyakazi wa Benki ya DTB, wawakilishi kutoka Vodacom, wadau mbalimbali wa soka pamoja na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Malinzi ameshukuru na kuupongeza udhamini huo uliotolewa na benki hiyo na pia ameziomba taasisi nyingine kuiga mfano huo ili kukuza soka nchini. “Kwa heshima ana furaha kubwa nawakaribisha DTB Tanzania kwenye ligi kuu na familia ya TFF kwa ujumla.”

Benki ya Diamond Trust ina matawi 25 nchini, ikiwa na matawi kumi na moja (11) jijini Dar es Salaam (Mtaawa Jamaat, Masaki, Morocco, Magomeni, Mbezi, Mbagala, barabara ya Nyerere, Msimbazi - Kariakoo, barabara ya Nelson Mandela, Upanga katika barabara ya umoja wa mataifa na katika makutano ya barabara ya Mirambo na mtaa wa Samora).

Vile vile ina matawi katika miji ya Arusha (2), Mwanza (2) na katika miji ya Dodoma, Kahama, Mbeya, Morogoro, Moshi, Mtwara, Mwanza, Tabora ,Tanga na Zanzibar.
DTB Tanzania ni mshirika wa mtandao wa maendeleo ya kiuchumi wa Aga Khan - Aga Khan Fund for Economic Development (AKFED) ambao ni sehemu ya mtandao wa maendeleowa Aga Khan Development Network).
DTB Kenya ni miongoni mwa wanahisa muhimu wa DTB Tanzania.

DTB Tanzania pia ni sehemu ya mtandao wa mabenki ya DTB Group yenye matawi zaidi ya 120 Afrika Mashariki na kati.

Ndeki's blog: GUARDIOLA AINGIA MTAANI NA KUJIACHIA NA MKEWE

Ndeki's blog: GUARDIOLA AINGIA MTAANI NA KUJIACHIA NA MKEWE: BAADA YA MWENDO BOMBA, GUARDIOLA AINGIA MTAANI NA KUJIACHIA NA MKEWE Sasa ulitaka afanye mini? Maana Kocha wa Man City, Pep Guar...

HUU SASA UCHOKOZI BARCELONA WANAMTAKA MWINGINE KUTOKA ARSENAL

Kuondoka kwa beki Dan Alves katika kikosi cha Barcelona bado ni pigo na ndiyo maana klabu hiyo imekuwa ikiendelea mchakato wa kutafura mchezaji sahihi anayeweza kuziba nafasi hiyo.

Beki wa kulia wa Arsenal, Hector Bellerin ametajwa kuwa ndiye anayongoza katika listi ya Barcelona katika dadi ya wachezaji wanaotakiwa kikosini hapo.

Hector Bellerin (kulia)





Mchezaji huyo amekuwa akifanya vizuri chini ya Kocha Arsene Wenger na hiyo ni moja ya sababu ambayo imemfanya Kocha wa Barcelona, Luis Enrique kuhitaji kumsajili.
Bellerin ambaye ana umri wa miaka 21 alizaliwa Barcelona na akaanza maosha yake ya soka akiwa na klabu hiyo kabla ya baadaye kuondoka akiwa katika kituo cha La Masia mwaka 2011, hivyo Barcelona wanataka kumrejesha nyumbani kijana wao kama ilivyokuwa kwa Cesc Fabregas.

GUARDIOLA AINGIA MTAANI NA KUJIACHIA NA MKEWE


Sasa ulitaka afanye mini? Maana Kocha wa Man City, Pep Guardiola mambo yanamuendea vizuri naye ameamaua kujiachia kiana.

Leo asubuhi ameonekana akiwa ana katikati ya mitaa ta jiji la Manchester akijiachia na mkewe Cristina Serra.


Pamoja na mkewe, Guardiola, kocha wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich aliongoza na kocha wa viungo ambaye ni memba wa benchi lake, Lorenzo Buenaventura.



Mwendo wa kikosi cha Man City chini yake unaonyesha uko safi na tayari ameanza kupewa nafasi ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England

Sunday, September 18, 2016

KILIMANJARO QUEEN YAFANYA KWELI YAUA 4-1,YATINGA FAINALI CHALENJI




Kikosi cha Kilimanjaro Queens kimetinga katika fainali ya Kombe la kwanza la Chalenji kwa wanawake baada ya kuwatwanga wenyeji wa michuano ya hiyo Uganda kwa mabao 4-1.

Uganda ambayo kikosi chao cha wanaume wakiwemo wachezaji kama Emmanuel Okwi kimefuzu kucheza Afcon, dada zao walionekana kuushindwa kabisa mziki wa Kilimanjaro Queens.

Ushindi huo sasa unaikutanisha Kilimanjaro Queens katika mechi ya fainali dhidi ya Kenya ambao wamefanikiwa kutinga baada ya kuwang’oa Ethiopia kwa kuwachapa mabao 3-2.

Katika mechi hiyo ya Kilimanjaro Queens mjini Jinja, wenyeji walionekana wamezidiwa kwa kiasi kikubwa na Queens walipata bao la mapema katika dakika ya 6 kupitia Donosia Daniel.

Kama vile wenyeji wangeweza kuamsha matumaini lakini walitandikwa bao la pili mfungaji akiwa Mwanahmisi Omari katika dakika ya 17 na Stumai Abdallah akapigilia msumari wa tatu dakika ya 31.

Kilimanjaro Queens walikwenda mapumziko wakiwa wanaongoza kwa mabao 3-0 na Asha Rashid ‘Mwalala’ alipigilia msumari wa mwisho huku wenyeji wakipata bao moja la ‘kuchafua gazeti’.

MOURINHO AWA MKALI,ASEMA NO KUPUMZIKA KESHO MAZOEZINI MAPEMA


Baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Watford kwa mabao 3-1, Kocha wa Manchester United amedai kuwa makosa binafsi ya wachezaji wake yamesababisha hali hiyo pamoja na kumtupia lawama mwamuzi katika bao la kwanza.





 Pamoja na kusema hivyo, amesisitiza kuwa vijana wake wote wanatakiwa kufika mazoezini kesho asubuhi na kuendelea na ratiba ya mazoezi huku muda wa kupumzika siku moja baada ya mechi kama ilivyo kawaida ukiwa haupo.


 

"Kesho tutakuwa na mazoezi saa 4.30 asubuhi, tunatakiwa kuwa pale ili kufanya kazi kuonyesha hatupo kwenye hali nzuri.

"Tunahitaji mawazo chanya ya kutuongoza ili mechi ijayo wakiingia uwanjani wajue tunaenda kufanya kazi gani."

Monday, August 22, 2016

TFF YAWASIMAMISHA WACHEZAJI WATANO 'VIMEO' LIGI KUU

Na John ndeki , DAR ES SALAAM

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limezitahadharisha klabu tano za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) juu ya kuwatumia wachezaji ambao imewasajili, lakini imebainika mbele ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kwamba wanamatatizo kwenye usajili wao.
Klabu hizo ni pamoja na Majimaji ya Songea ambayo ina mchezaji anayefahamika kwa majina ya George Mpole ambaye pia amebainika kuwa ndiye Gerald Mpole wa Majimaji ya Songea amefungiwa kucheza soka kwa mwaka kwa kosa la kubadili jina akiwa na lengo la kufanya udanganyifu kwenye usajili. Majimaji imeagizwa kutomtumia mchezaji huyo kutoka Kimondo FC.
Mwadui FC ya Shinyanga; Mchezaji William Lucian aliyesajiliwa na Mwadui ya Shinyanga kutoka Ndanda ya Mtwara, naye amefungiwa mwaka mmoja kwa kosa la kusajili Mwadui FC ilihali akiwa hajamaliza mkataba na Ndanda. Mwadui isimtumie mchezaji huyo.
Mbeya City ya Mbeya; Mchezaji Saidi Mkopi, pia amefungiwa mwaka mmoja kwa kosa la kujisali timu mbili. Imebainika kuwa akiwa bado na mkataba na Tanzania Prisons ya Mbeya hivyo Mbeya City isi1mtumie mchezaji huyo.
African Lyon ya Dar es Salaam; Mchezaji Rehani Kibingu aliyesajiliwa na African Lyon ya Dar es Salaam, amesimamishwa kuchezea timu hiyo mpaka uongozi wa African Lyon kumalizana na Ashanti United ya Dar es Salaam kabla ya Agosti 27, 2016. African Lyon isimtumie mchezaji huyo kwa sasa.
Mbao FC ya Mwanza; Mchezaji Emmanuel Kichiba aliyesajiliwa Mbao FC, naye amesimamishwa mpaka Mbao watakapomalizana na Ashanti United ya Dar es Salaam, kabla ya Agosti 27, 2016. Mbao FC isimtumie mchezaji huyo kwa sasa.

FIFA YAWAPA KOZI YA UTIMAMU WA MWILI MAKOCHA WA TANZANIA


Na JOHN NDEKI, DAR ES SALAAM
SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA), kwa mara nyingine limeipa nafasi Tanzania kwa kutoa kozi maalumu ya utimamu wa mwili (Physical fitness) kwa makocha wa Tanzania wenye leseni kiwango B inayoanza leo Agosti 22, 2016. Kozi hiyo inayoendeshwa na mkufunzi kutoka FIFA, Dk. Praddit Dutta, raia wa India itafikia ukomo Ijumaa wiki hii.
Akifungua kozi hiyo, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine aliishukuru FIFA kwa namna inavyoipa nafasi Tanzania katika kozi mbalimbali hususani za ukocha na uamuzi.
“Si kila nchi inapata privilege (fursa) kama hii. Bila shaka FIFA inatambua uwezo wa makocha wa Tanzania kwa sasa. Mjue kuwa FIFA ina watu wa kuwapa taarifa kila kona. Kama mngekuwa mnafanya vibaya, FIFA wangesema Tanzania bado, kwa hiyo kozi zisipelekwe… lakini inaonekana mnafanya vema, mngefanya vibaya msingefikiriwa,” alisema Mwesigwa aliyekuwa mgeni rasmi katika ufunguzi huo.
Mwesigwa amesema kwa kuwa FIFA ina malengo chanya na Tanzania kwa kutoa kozi mbalimbali ikiwamo hiyo ya physical fitness inayolenga kuwapa ujuzi makocha hao kuwajengea uwezo wachezaji kuwa na stamina.
Hivyo akawataka makocha wanaohudhuria kozi hiyo kutumia fursa hiyo ya mafunzo si kwa ajili yao peke yao bali kuendeleza ujuzi huo kwa wengine ambao hawakubahatika kuwa sehemu ya wateule wa FIFA.
Naye, Mkufunzi wa kozi hiyo, Dk. Dutta alisema: “Bila shaka Tanzania inakwenda kufungua ukurasa mwingine wa soka la weledi kwa kuwa na wataalamu mbalimbali katika ukocha na uamuzi. Mnachotakiwa ni kujitahidi kufanya vema na kozi nyingine nyingi zinakuja.”
FIFA kwa kushirikiana na Idara ya Ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), chini ya Mkurugenzi Salum Madadi, imepitisha majina ya makocha 27 kuhudhuria kozi hiyo inayofanyika katika Hosteli ya TFF iliyoko kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

Makocha wanashiriki kozi hiyo ni Mohammed Muza, Samwel Moja, Nassa Mohammed, Jemedari Said, Oscar Mirambo, Wane Mkisi, Cletus Mutauyawa, Shaweji Nawanda, Kizito Mbano, Dennis Kitambi, Sebastian Nkoma, Fikiri Mahiza, Nyamtimba Muga, Nassor Mwinchui, Alfred Itaeli, Henry Ngondo, John Tamba, Kidao Wilfred, Luhaga Makunja, Mohammed Tajdin, Mohammed Silima, Salum Ali Haji, James Joseph, Kessy Mziray, Daudi Sichinga, Bakari Shime na Salum Mayanga.