Powered By Blogger

Thursday, July 7, 2016

RONALDO AIFIKIA REKODI YA PLATINI


Pamoja na kuiongoza Ureno kushinda mabao 2-0 dhidi ya Wales na kutinga fainali ya Euro 2016, Cristiano Ronaldo amefunga bao lake la 9 katika michuano ya Euro.

Bao hilo la 9, maana yake amemfikia mfungaji bora wa miaka yote wa michuano ya Euro, Michell Platini wa Ufaransa.


Ronaldo amebakiza mchezo mmoja dhidi ya kati ya Ujerumani au wenyeji Ufaransa. Kama atafunga basi atakuwa ameweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Euro.

URENO WATINGA FAINALI YA EURO WAICHAPA WALES 2-0

johnndeki.blogspot.com


Cristiano Ronaldo amefunga bao moja na kutengeneza moja na kuiwezesha Ureno kutinga fainali ya Euro kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wales.

Ronaldo ndiye alifunga bao la kwanza katika dakika ya 50 na kusababisha la pili lililofungwa na Louis Nani na kuzima ndoto za Wales iliyokuwa ikiongozwa na Gareth Bale anayekipiga timu moja ya Real Madrid na Ronaldo.

Awali, kulikuwa na ubishi, nani kati ya Ronaldo na Bale atatinga fainali. Ingawa Bale alionyesha kiwango bora kabisa lakini sasa jibu liko hadharani.

Hadi inatinga nusu fainali, haikuwa imeshinda hata mechi moja ndani ya dakika 90. Pia ilivuka hatua ya makundi ikiwa best looser.

Leo imeshinda kwa mara ya kwanza ndani ya dakika 90 na kufanikiwa kutonga fainali.



















Wednesday, July 6, 2016


Kipa wa zamani wa Tenerife ya Hispania, Juan Jesus Gonzalez amesema yuko tayari kwa ushindani licha ya kwamba ni mara yake ya kwanza kucheza barani Afrika.

Jesus yuko nchini kwa ajili ya kufanya majaribio ili ajiunge na Azam FC kwa ajili ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza leo na SALEHJEMBE, Jesus amesema matarajio ya ushindani mkubwa ni jambo jema kwake.

"Nataka kushindana na kufanya vizuri, najua Azam ni timu kubwa Tanzania. Nitaonyesha uwezo wangu," alisema akionyesha kujiamini.

Kipa huyo mtaratibu, ametua nchini tayari kwa ajili ya kujiunga na Azam FC kama watakubaliana na uongozi wa klabu hiyo ambayo ndiyo mpinzani mkubwa wa watani Yanga na Simba.

MANENO YA MOURINHO BAADA YA KUTUA MAN UNITED


Kocha mpya wa Man United, Jose Mourinho amesema maneno kadhaa mara tu baada ya kukabidhiwa kikosi hicho kwa kutangazwa mbele ya waandishi.

Katika shughuli hiyo ya kutangazwa leo, Mourinho amesisitiza suala la kuhakikisha Man United inakuwa timu inayofuzu kwa uhakika kucheza michuano ya kimataifa hasa Ligi ya Mabingwa.

Lakini amesisitiza atakuwa ni mtu mwenye kufanya maamuzi magumu bila ya uoga.

Kilichowavutia wengi, ni baada ya Mourinho kusema anahitaji kila kitu na kama inawezekana ni kushinda mataji yote.

TAKWIMU:
UMRI: 53
CLUB ALIZOFUNDISHA:
2000 Benfica
2001-02 Uniao de Leiria
2002-04 Porto
2007-07 Chelsea
2008-10 Inter Milan
2010-13 Real Madrid
2013-15 Chelsea
2016-present Manchester United
Honours:
Champions League x2
UEFA Cup x1
Premier League x3
FA Cup x1
League Cup x3
La Liga x1
Spanish cup x1
Serie A x2
Italian cup x1 
Portuguese league x2
Portuguese cup x1 





AZAM FC YASHUSHA KIPA MPYA


Uongozi wa Azam FC umeamua hasa, baada ya kumshusha kipa kutoka Tenerife ya Hispania, sasa kuna kipa wa timu ya taifa ya Ivory Coast.

Huyu ni Daniel Yeboah Tetchi ambaye yuko jijini Dar es Salaam tayari kumalizana na Azam FC ili aitumikie msimu ujao.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 31, alianza kuonyesha cheche zake akiwa Asec Mimosa ya Ivory Coast.
Pia amewahi kuitumikia Dijon ya Ufaransa katika kikosi chake cha pili.


Habari za uhakika zinaeleza, Tetchi yuko katika nafasi kubwa ya kumalizana na Azam FC lakini suala la kipa Mhispania linaweza kuweka ushindani mbele yake.

HATIMAYE HATIMA YA PISTORIUS YAPATIKANA

www.johnndeki.blogspot.com
HATIMAYE IMEFIKIA MWISHO, PISTORIUS AFUNGWA MIAKA SITA JELA

Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius amefungwa jela miaka sita na atarejea uraiani mwaka 2019.

Pistorius amefungwa baada ya kupatikana tena na hatia ya kuua mpenzi wake Reeva Steenkamp mwaka 2013.

Jaji Thokozile Masipa aliyemhukumu, amesema mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 29 amepewa nafasi ya kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

MUONEKANO MPYA WA WANYAMA

WWW.JOHNNDEKIBLOGGSPORT.COM


Tayari kiungo Mkenya, Victor Wanyama ameanza mazoezi na kikosi chake kipya cha Tottenham ya England.

Mkenya huyo amejiunga na Spurs akitokea Southampton. Cheki picha.



VODACOM YAMWAGA SH MILIONI 6



Kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom imetoa Sh milioni 6 kudhamini safari ya mafunzo ya wahariri 30 wa michezo nchini ambao wanakwenda nchini Kenya.

Wahariri hao kupitia Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa) ambao wamepata mwaliko kutoka kwa chama cha Kenya (SJAK), watakwenda jijini Nairobi kwa ziara hiyo ya mafunzo.

Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom, Jacqueline Materu amesema: “Tumeona hii ni fursa njema kusaidia ziara hiyo ambayo itakuwa na faida katika maendeleo ya tasnia ya habari pamoja na michezo.”


Kwa upande wa Taswa, Makamu Mwenyekiti, Egbert Mkoko aliwashukuru Vodacom kwa udhamini huo ambao alisema wameonyesha undugu wa damu.




ARSENAL WAANZA MAANDALIZI YA MSIMU UJAO WA LIGI KUU YA ENGLAND



Pamoja na kwamba inawakosa baadhi ya wachezaji wake wanaoshiriki michuano ya Euro Arsenal imeanza maandalizi ya Ligi Kuu England.

Walio katika michuano ya Euro baada ya timu zap kufuzu hatua ya nusu fainali ni Aaron Ramsey, Mesut Ozil, Olivier Giroud na Laurent Koscielny.

Lakini wengine wameanza maandalizi ya msimu mpya chino ya Kocha Arsene Wenger.









sibuka fm


  • sikiliza sibuka fm online kupitia www.sibukafm.co.tz mwanza 95.5 fm 94.5 fm dar es salaam 97.0 fm maswawww.johnndeki5@gmail.com