Powered By Blogger

Friday, August 19, 2016

DIDDY NA CASSIE WAMWAGANA

``Diddy na Cassie wamwagana kwa ugomvi mkubwa, polisi waitwa

`Diddy na Cassie wameachana rasmi kufuatia ugomvi mkubwa uliozuka kiasi cha kuwafanya polisi waende nyumbani kwao, wa mujibu wa mtandao wa TMZ.

Vyanzo vilivyo karibu na wawili hao, vimeuambia mtandao huo kuwa yalizuka mabishano makali kati yao wakiwa kwenye gari Jumatano mchana baada ya Cassie kumwambia Diddy kuwa anataka waachane. Wamesema kuwa Diddy alikasirika kiasi cha kushika simu yake na kuanza kuangalia vitu vilivyomo.
Vyanzo hivyo vimesema kuwa Diddy aliruka kutoka ndani ya gari huko Bev Hills akiwa na simu mkononi na Cassie kuondoka na dereva.
Hatimaye Diddy alirejea nyumbani na kuipeleka simu lakini baadaye akachukua magari mawili yaliyokuwa yameegeshwa nje.
Cassie alikuwa amemuambia mama yake kuhusu tukio la simu kabla Diddy hajarejea nyumbani na kuirejesha na hivyo aliwaita polisi. Polisi walifika nyumbani kwa Cassie na kuwaeleza kuwa ameipata simu yake na wakaondoka japo waliandika ripoti ya tukio hilo. Hata hivyo hakuna kosa lililofanyika.
Kuhusu kuachana, wawili hao wamewahi kuachana kabla.

No comments:

Post a Comment