ULE MKATABA WA TFF NA DIAMOND TRUST ISHU IKO HIVI...
Benki
ya Diamond Trust (DTB) leo imesaini kuingia mkataba na Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) kudhamini Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (VPL) kwa
msimu wa mwaka 2016/2017.
DTB
inaungana na mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) pamoja na wadhamini wengine
katika kudhamini ligi hiyo maarufu kama Ligi Kuu ya Vodacom.
Akizungumza
na waandishi wa habari kwenye hafla ya utiaji saini huo iliyofanyika
Hoteli ya Serena, Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki hiyo, Joseph Mabusi
amesema: “Udhamini huu utasaidia zaidi maendeleo ya soka nchini kwa
kuziwezesha timu timu shiriki pamoja na jitihada zingine za TFF. Soka
inaunganisha Watanzania wa matabaka mbalimbali ambao ni wateja wetu na
si kama benki tungependa kuwa karibu nao zaidi kupitia mchezo huu.”
Mabusi
aliongeza kwa kusema: “Tunafurahi na kujivunia kuwa sehemu ya ligi kuu
na tunaamini udhamini huu utazidisha ari ya kuwahudumia Watanzania
wote.
Benki
ya Diamond Trust imekuwa ikiipa kipaumbele michezo mbalimbali ikiwemo
soka, ambapo timu rasmi ya soka inayoundwa na Wafanyakazi imefanikiwa
kushinda vikombe na mataji mbalimbali ya soka likiwemo taji la ligi ya
mabenki nchini inayojulikana kama BRAZUKA KIBENKI mwaka 2015 pamoja na
ngao ya hisani ya ligi hiyo mwaka 2016.
Benki
pia inadhamini timu ya soka ya Agathon iliyopo Mbagala inayoshiriki
ligi soka daraja la tatu. Zaidi ya hayo benki pia inajivunia kuwa moja
kati ya wadhamini wa michuano ya CECAFA Kagame Cup mwaka 2015.
Ligi
hiyo inajumuisha timu 16 kutoka Tanzania bara zinazocheza kwa mfumo wa
mechi za nyumbani na ugenini ambazo ni Young Africans, Simba Sports
Club, Azam FC, Mtibwa Sugar, Kagera Sugar, Mbeya City, Majimaji, MbaoFC,
African Lyon, JKT Ruvu, Ruvu Shooting, Tanzania Prisons, Stand United,
mwadui FC, Ndanda FC na Toto Africans.
Hafla
hiyo ilihudhuriwa na viongozi waandamizi wa Shirikisho la Soka Tanznaia
–TFF wakiongozwa na Rais wao Ndugu Jamal Malinzi, Wafanyakazi wa Benki
ya DTB, wawakilishi kutoka Vodacom, wadau mbalimbali wa soka pamoja na
waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Malinzi
ameshukuru na kuupongeza udhamini huo uliotolewa na benki hiyo na pia
ameziomba taasisi nyingine kuiga mfano huo ili kukuza soka nchini. “Kwa
heshima ana furaha kubwa nawakaribisha DTB Tanzania kwenye ligi kuu na
familia ya TFF kwa ujumla.”
Benki
ya Diamond Trust ina matawi 25 nchini, ikiwa na matawi kumi na moja
(11) jijini Dar es Salaam (Mtaawa Jamaat, Masaki, Morocco, Magomeni,
Mbezi, Mbagala, barabara ya Nyerere, Msimbazi - Kariakoo, barabara ya
Nelson Mandela, Upanga katika barabara ya umoja wa mataifa na katika
makutano ya barabara ya Mirambo na mtaa wa Samora).
Vile
vile ina matawi katika miji ya Arusha (2), Mwanza (2) na katika miji ya
Dodoma, Kahama, Mbeya, Morogoro, Moshi, Mtwara, Mwanza, Tabora ,Tanga
na Zanzibar.
DTB
Tanzania ni mshirika wa mtandao wa maendeleo ya kiuchumi wa Aga Khan -
Aga Khan Fund for Economic Development (AKFED) ambao ni sehemu ya
mtandao wa maendeleowa Aga Khan Development Network).
DTB Kenya ni miongoni mwa wanahisa muhimu wa DTB Tanzania.
DTB Tanzania pia ni sehemu ya mtandao wa mabenki ya DTB Group yenye matawi zaidi ya 120 Afrika Mashariki na kati.
No comments:
Post a Comment